Sunday, July 15, 2012

0 JIMWAGE, Please Advise Me

Habari Gracella,

Kwanza kabisa nashukuru sana kwa kuanzisha hii segment ya jimwage, yani imekuja on the right time kwani nina utata moyoni na siwezi kumhadithia ndugu yangu wala rafiki kwani maneno maneno sipendelei na  nilishaumizwa sana na marafiki mpaka siamini tena kumpa mtu siri yangu.
Mimi ni msichana wa miaka 29, japo nipo mkoani ila ni mpenzi mzuri sana wa blog yako kwani inanihabarisha fashion trends ambazo ziko current c unajua tena mkoa.  Tatizo langu nina wapenzi au niseme wachumba wawili na wote wapo serious na wanataka kuleta posa nyumbani yani im so confused kwani mwanzo nilijua ts a joke nilikuwa serious na boyfriend wangu wa kwanza huyu wapili alikuwa kama mtu wangu tu endapo huyu akiniumiza.

BF wangu wa kwanza  yupo dar na nilianza nae toka niko secondary form three na yeye ndo mwanaume wangu wa kwanza. Sio siri nampenda sana kwani anasifa zote nnazotaka kwa mwanaume kimuonekano sema huwa ananiumiza mara nyingi. He hardly has time to go out, kila mara yupo busy tu, nikimuuliza anasema anatafuta pesa(ni Mchagga). Pia nilishamfumania na msichana mdogo akaniomba msamaha nikajua yameisha ila akaendelea nae mpaka akampa mimba.
Niliumia sana na hivi sasa mtoto huyo ana miaka miwili, ila he claims that wameachana kabisa na huyo mzazi mwenzie na uhusiano pekee ulobaki  kati yao ni juu ya matunzo ya huyo mtoto.
Mchumba wa pili nilianza nae nilipokuja huku Mkoani after being frustrated na kuumizwa sana na my first BF. Nilianza nae kimzaha mzaha tu, cha ajabu I fell in love with him. Kiukweli yeye hana mvuto nnaoutaka mimi; pia hana hela sana sana anazakubadilishia mboga tu (yani mwenzangu na mie)  sema he is  so so sweet, ananijali na anasifa zote za mwanaume mzuri, ( A Husband Material).
Mwaka huu mwezi wa nne my  1st BF alikuja; we had all the fun na akasema kwamba anataka kunioa na yupo serious, kwani amegundua im the only woman for him. Nilijua utani ila kweli yuko serious na suala zima la ndoa.  Na kwa upande mwingine huyu 2ND Bf nae amekuwa akitaka kufika nyumbani muda kwa muda mrefu sasa ila nikawa nnamzuga kwani even though nawapenda wote najua nampenda zaidi huyu wakwanza japo yuko hivyo ila nadhani ndo mwanaume wa kuniridhisha.

Please naomba mnishauri kwani kuolewa nataka, na nnampenda sana tha 1st BF. Ila pia kuna vitu naogopa na huwa nnajiuliza kwamba, je? nikijateseka by his characters japo anaonesha kuwa amebadilika, yani he is more caring since February mwaka huu na pia sitaki kumkosa the 2nd BF.

Please nishaurini; nipo tayari kupokea mawazo yenu.

Desperate House Wife.

0 comments:

Total Pageviews

Members

 

Flexy Collections Copyright © 2011 - |- Template modified by Edward Lila 0715 574363r - |- Powered by Blogger Templates